MAJALIWA: HAKUNA MTU ALIYELAZIMISHWA KUCHANJA CHANJO YA UVIKO 19

*Awataka wananchi wapuuze upotoshwaji unaoendelea mitandaoni WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haijamlazimisha na wala haitamlazimisha mwananchi kuchanjwa chanjo ya ugonjwa wa UVIKO 19, hivyo amewataka Watanzania wapuuze upotoshaji unaosambazwa kupitia mitandao ya kijamii.  “Hakuna aliyelazimishwa kuchanja chanjo hiyo na wala hakuna mahali palipoandikwa kwamba lazima wananchi wachanjwe. Chanjo ni hiari tusipotoshane kwa sababu hakuna